Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +25565373432 | +255778744123 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Wednesday, 4 January 2017

RSA NI IBADA Mhe. Perreira Silima (NW-MN) 2015


Mhe. Perreira Silima - Naibu Waziri Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani

Mhe. Perreira Silima - Naibu Waziri Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani akiielezea RSA
“......kama mna dini, mnachofanya kwenye mambo haya ni ibada, kuokoa maisha, kuzilinda familia zisije zikaparaganyika,kwa sababu baba kafariki au mama kafariki ajli, au wakati mwingine hata kupata majeruhi na ulemavu wa kudumu ni tatizo. Kwa hiyo hili jambo tunalolifanya, na uziri ninyi mlioamua kulifanya mnafanya kwa ridhaa na kufurahi, na hicho ndicho kitakachotusaidia kwa sababu kina hamasa binafsi. Sisi wengine, mimi keshokutwa naweza kwenye uchaguzi nikawa sipo lakini naweza nikabaki [RSA] kwa sababu ya uhamasikaji wangu, lakini leo pengine nahamasika kwa sababu ni sehemu ya kazi yangu. Mpaka nitakapokuwa siko hapa, mkiniona sipo hapa, mkiniona sijaondoka kwenye bunge mtajua kwamba nami nimehamasika kweli kweli kwa nafsi yangu. Nawashukuru sana sana kwa uamuzi wenu wa kujiunga na sisi......Na ukiangalia hata sisi wenye jukumu la kupunguza ajali, hivi sasa tuna wigo mpana, kuna mtu atatuambia huyu hapa ametanua....Kwa sababu ni hiyari na uchungu ndani, hata sisi nimeona several times mnatukosoa na mnatuonesha kwamba mmoja wenu huyu anafanya visivyo na hili jambo kwa kweli in the long run na tukaendelea kuwa wengi basi tutakuwa na udhibiti mzuri kwenye ajali.
Na kama mlivyosema, ninyi mna kazi zenu na mna majukumu ambayo mlitakiwa muyafanye, lakini kulifanya hili nal jukumu lenu kwa ridhaa ni jambo zuri. Kunwa wafanyabiashara mnaacha shughuli zetu, kuna wafanyakazi, pengine mngekuwa na familia,...lakini mmejitoa mkasema wacha twende Dodoma tukaonenkane kama RSA tuwawakilishe wenzetu na mmekuja tunashukuru. Kuna watu wamejua kwamba RSA is there na wengine wataendelea kuhamasika taratibu. Kwa sababu, pamoja na kuwa tunajitangaza, lakini bado tunajitanaza narrowly mahala ambapo pengine ni wataalamu tu wanaweza kufika kwenye telegram, au kwenye whatsapp au kwenye facebook kwenye the plethora ya Tanzanians hawajui kama tupo tunaexist. sasa watu wengi waangalia bunge siku hizi, kuna wengine hawajaelewa wakiambiwa mabalozi, mabalozi itaendelea kuwa masuala ambayo yatawasumbua mwisho watakuja kuelewa.

Ninachowaomba tu muendelee kuwa na uchungu na jambo hili, tuendelee kushikamana, tuendelee kulipanua na tutafanya impact, na hilo ndilo jambo ambalo tunataka tuachieve. Sasa mmi furaha yangu ni kuwa kuwa part ya RSA, mnatuwakilisha, na you are really ambassadors from nowhere. Hii ni initiative ambayo ipo sasa, i believe kutakuwa na nyingine nyingi zitatokea za kupashana habari, za kuwajibishana mpaka tuone kwamba tatizo hili kubwa tulilonalo la janga la accident linapungua. Tanzania ukiwatajia malaria, ukiwatajia UKIMWI, kuna NGOs nyingi zinapata hela from everywhere lakini tulipofikia janga la malaria na UKIMWI unaweza ukaliona kama dogo kuliko la ajali za barabarani ambalo bado halijapata that profile. Sasa the onus is upon us, sisi ambao tayari tumeanza kuona kwamba hili jambo ni muhimu na kuanza kulifanyia kazi.
Mimi naamini tutakuwa na tutakuwa na shape tofauti as time goes na hiyo ndiyo itakayosaidia Tanzania kubadilika na kupunguza hii shida tuliyonayo. Kwa kweli nimefurahi sana. Kuna mtu aliniambia kamanda, sijui Ulinambia yuko Uholanzi...(eeh Fungo yupo uholanzi anasoma) eeh Fungo in fact ndio aloanza kuniconnect kwenye hii safari yenu am happy kwamba imefanikiwa. Mwanzoni kama wengine hatukuamini kwa resoure hizi...lakini tumeweza. Niwapongeze wale ambao, apart from kujitoa lakini pia wakajitoa zaidi mmetusaidia na kama tulivyosema ni kazi ya hiyari. Kazi ya hiyari siku zote ina maumivu kwako, si maumivu kwa maana ya maumivu lakini ina effect ya namna fulani unaifeel wewe unapopunguza bajeti yako, unapopunguza wakati kwenye shughuli zako na vitu kama hivyo.

Kwa hiyo am pleased kwamba mnafanya kazi ya ubalozi na you are really doing it well. Tuendelee kujiimarisha ili lengo la kujianzisha kwetu lizidi kuwa na matunda. Nawashukuru pia kuja kuniona, at least na weza kujua admin4, Seka from today. I always read lakini siwezi kujua nani ni nani, who is Seka? I thought Seka is an Indian..Yaani imenisaidia nawashukuru sana…”
Perreira Silima-23rd May, 2015