Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +25565373432 | +255778744123 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Tuesday, 28 March 2017

Mpinga asema; Tanzania imepata mafanikio makubwa katika kuthibiti ajali za barabarani.

 Kamanda wa kikoai cha usalama wa barabarani DCP Mohamed Mpinga akizungumza katika hafla ya kufunga kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyofanyika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, ambapo kampeni hiyo ilizinduliwa Novemba 2016 na Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Hamad Masauni ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani Tanzani.
 
Na. Vero Ignatus & Murtadhwa Elbahsan Dar es salaam. 

Madereva wa mabasi makubwa yaendayo mikoani wameaswa kutokuchezea mfumo wa kufuatilia mwenendo wa mabasi haswa mwendo kasi ,yeyote atakae bainika ameuharibu hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Mohamed Mpinga  katika hafla ya kufunga kampeni ya abiria paza sauti iliyofanyika katika  katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo ambapo amesema kuwa mwendo kasi ni chanzo kikubwa cha ajali barabarani 

Kamanda amefafanua kuwa kampeni hiyo imeleta matokeo chanya ambayo imeonyesha kupungua kwa ajali ukilinganisha na miaka 25 iliyipita  nakusema kuwa Tanzania imepata mafanikio makubwa katika kuthibiti ajali za barabarani .

Amezitaja takwimu hizo kuanzia mwaka  2015 Desemba ajali zilikuwa 767 , Disemba 2016 ajali zilikuwa 705, ambapo januari 2016 ajali zilikuwa 681 hadi januari 2017 ajali zilikuwa 525, Februari 2016 ajali zilikuwa 846 ambapo februari 2017 ajali zilikuwa 455 ,kuna upungufu wa asilimia 46 'ambapo ajali zinazidi kupungua mwaka hadi mwaka. 

Ameendelea kusema kuwa kwa takwimu hizo hadi sasa Tanzania imepiga   kubwa katika kudhibiti ajali za barabarani na hii ni takribani nusu karne tangia mwaka 1989.
 
Kamanda Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na Madereva waliopendekezwa kama madereva bora 2016 - 2017 katika hafla ya kufunga kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyofanyika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, ambapo kampeni hiyo ilizinduliwa Novemba 2016 na Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Hamad Masauni ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani Tanzani.
 
Vile vile Kamanda mpinga alitoa vyeti vya pongezi kwa madereva walio pendekezwa kama madereva bora kwa mwaka 2016 - 2017 ambao ni;
1. AWADH BAWAZIR(RATCO).
2.ALLY ISSA (STAR BUS)
3. MUSTAPHA GHARIB(KIMBINYIKO)
4. DAUDI LWENA(KHANDAHAR). 
5. MENGI KASIKE(SUTCO).
6. MAJURA KAFUMU
 
Kwa upande wake mratibu na mwenyekiti wa abiria paza sauti  Asp.Mosi Ndozero  amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa madereva pamoja na wahudumu  wa magari sambamba na kuwaelimisha abiria kufahamu haki zao pia kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale wanapoona viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani ambavyo vinaweza kusababisha ajali na kupoteza maisha au ulemavu wa kudumu.

 Mosi amesema kuwa mtu anapopata ajali haathiriki yeye peke yake inajumuisha familia yake pamoja na serikali kuingia gharama kubwa ya  kumuuguza huyu mtu  aliyepata ajali,amewataka mabalozi kuendelea kupaza sauti kwa madereva bodaboda ambao wanapakiza mizigo kuzidi uwezo wa pikipiki pamoja na wale anaopakia Mishikaki.
 
Asp. Mosi Ndozero Mwenyekiti wa Kampeni ya Abiria Paza Sauti akizungumza katika hafla ya kufunga kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyofanyika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, ambapo kampeni hiyo ilizinduliwa Novemba 2016 na Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Hamad Masauni ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani Tanzani.
Picha na Vero Ignatus & Murtadhwa Elbahsan