Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +25565373432 | +255778744123 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Wednesday, 19 April 2017

RSA - Zanzibar: Balozi Seif Ali Iddi Azindua Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Zanzibar............... Ashauri Sheria za Usalama Barabarani Ziongezwe Makali.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akionyesha cheti maalum baada ya kuweka saini yake cha kuthibitisha uzinduzi rasmi wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Zanzibar (RSA) hapo Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar. Wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Kamishna wa Kikosi cha Usalama Bara barani Tanzania DCP Mohamed Mpinga, Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Waziri wa Ujenzi Balozi Ali Karume na Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Hamdan Makame.


 Na Murtadhwa Elbahsan, Zanzibar.

 Matukio ya uvunjifu wa sheria za usalama Bara barani bado yanaendelea kupoteza nguvu kazi ya Taifa wakiwemo Vijana wazee na watoto huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu na wengi kuendelea kuwa mayatima katika maisha yao yote.

Akizindua rasmi Mtandao wa Mabalozi wa wa Usalama Bara barani Zanzibar hapo ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi alisema hali hiyo imeendelea pia kuleta hasara kwa Taifa kutokana na kuharibiwa kwa miundombinu ya Bara bara na vifaa vyengine.

Balozi Seif alisema ajali za bara barani bado zimekuwa ni tishio kwa maisha ya wannchi kutokana na baadhi ya madereva ama kwa makusudi kutotii sheria na taratibu zilizowekwa katika kufuata matumizi sahihi yaliyowekwa bara barani.

Alisema baadhi ya madereva hao wamekuwa na tabia ya kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo wa kasi bila ya kujali watumiaji wengine mbali mbali kama watoto ambao nao wana haki ya matumizi ya bara bara hizo.

Balozi Seif alionyesha masikitiko yake kutokana na baadhi ya madereva ambao husababisha ajali za kizembe kutokana na ustaarabu wa kisasa ulioingiza wa kuendesha chombo cha moto na huku wanazunguza na simu wakati mataifa mengine Duniani hili wanalihesabu kuwa kosa kubwa bara barani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema uamuzi wa kuanzishwa kwa dhana hii ya mabalozi wa usalama Bara barani hapa Zanzibar ni wa busara na kuwa wakati muwafaka ambapo Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada za kukabiliana na ajali za bara barani.
 

  Mapema akitoa Tarifa Mwenyekiti wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani Nd. Mustafa Mussa alisema Mtando huo wa Kiraia umeanzishwa kwa lengo la kulisaidia Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama bara barani kupambana na na makosa yanayotokana na bara bara.

Naye Mlezi wa Mabalozi wa usalama Bara barani Msaidizi Kamishna wa Jeshi la Polisi (ACP ) Mkadam Khamis Mkadam alisema ajali nyingi zinazotokea Bara barani hutokana na vitendo visivyo tii sheria za usalama bara barani.

Alisema ajali za bara barani zilizotokeza mwaka 2016 zilifikia mia 604 na kusababisha vifo vya watu 147 wakati mwaka 2017 ziliripotiwa ajali mia 517 zilizosababisha vifo vya watu 133 kukiwa na upungufu wa vifa vya watu 14.

 


Balozi Seif akimkabidhi cheti Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Bibi Narsa Mohamed kutokana mchango mkubwa uliotolewa na vyombo vya habari vya Shirika hilo wa suala la usalama bara barani.
Balozi Seif akikabidhi cheti maalum kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani Tanzania Bwana John Seka kutokana na mchango mkubwa wa Taasisi hiyo uliosaidia kupunguza ajali za vyombo vya moto Bara barani Tanzania Bara.


Picha na – Elbahsan Blog ZNZ.

Tuesday, 18 April 2017

RSA YAZALIWA ZANZIBAR LEO --- 18-04-2017

Mabalozi wakiwa Bandarini tayari kwa safari ya kuelekea Zanzibar kwenye uzinduzi wa RSA Zanzibar.Na. Murtadhwa Elbahsan, Dar es saalm
Viongozi wa RSA wafunga safari kwenda kuzindua RSA Zanzibar leo tarehe 18/04/2017. Msafara huo ukiongozwa na DCP Mohammed Mpinga (Mlezi wa RSA Tanzania) pamoja Mwenyekiti wa RSA Nd.John Seka

Baada ya miaka 3 ya RSA Tanzania Bara, leo hii RSA itazinduliwa rasmi huko Tanzania Visiwani (Zanzibar) kwa lengo la kukuza taasisi lakini pia kuwafikia watanzania wote ili kuwa chachu ya kuondoa ajali nchini, RSA imekua ikijikita katika utoaji wa elimu za usalama barabarani lakini pia kuhusu masuala ya bima, kwa wamiliki wa vyombo vya moto na watumiaji wa vyombo vya moto (Abiria). 

Mapema leo hii RSA itazinduliwa rasmi Visiwani Zanzibar na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanziba Mh. Balozi Seif Ally Iddi, katika ukumbi wa Baraza la wawakilishi Unguja. Sherehe hizo za uzinduzi zitafnyika kuanzia Saa sita mchana leo hii.


DCP Mohammed Mpinga (lezi wa RSA) akiwa na Viongozi wa RSA Taifa kwenye Boti wakielekea Zanzibar kwaajili ya uzinduzi wa RSA.


Mabalozi wakibadilishana mawazo wakati wa safari ya kuelekea Zanzir


Mabalozi wakiwa ndani ya boti wakielekea Zanzibar
Mabalozi wakiwa ndani ya boti wakielekea Zanzibar

>>>>> Tujikumbushe

RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani. Motto wa RSA: "USALAMA BARABARANI NI HAKI NA JUKUMU LETU SOTE"

Taasisi hii ilianzishwa 17.12.2013. Malengo ya  RSA kwa ujumla ni:
1. Kufanya kazi kama trafiki jamii kwa kuripoti matukio yote ya uvunjifu wa sheria za babarani.
2. Kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama barabarani
3. Kuelimishana RSA kwa RSA kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo usalama barabarani na bima
4. Kuwa chachu ya mabadiliko ya sera, sheria za usalama barabarani, mienendo na tabia za askari na madereva barabarani.
5. Kuwa mfano wa kuigwa(balozi) wa kutii bila shuruti sheria na taratibu za Usalama barabarani.
6. Kushirikishana uzoefu kutoka mahali mbalimbali duniani kuhusu usalama barabarani.
7. Kutumia majukwaa ya RSA kama sehemu ya kuuliza maswali, kujibu maswali, na kujadili masuala mbalimbali yahusuyo usalama barabarani.
8. Kupeana taarifa mbalimbali kuhusiana na usalama barabarani na hali ya barabara.


Taasisi hii inamakundi yaliyopo whatsapp yanayoitwa RSA-KULIKONI BARABARANI.

Sunday, 16 April 2017

Mpinga asema; Tanzania imepata mafanikio makubwa katika kuthibiti ajali za barabarani.

 Kamanda wa kikoai cha usalama wa barabarani DCP Mohamed Mpinga akizungumza katika hafla ya kufunga kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyofanyika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, ambapo kampeni hiyo ilizinduliwa Novemba 2016 na Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Hamad Masauni ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani Tanzani.
 
Na. Vero Ignatus & Murtadhwa Elbahsan Dar es salaam. 

Madereva wa mabasi makubwa yaendayo mikoani wameaswa kutokuchezea mfumo wa kufuatilia mwenendo wa mabasi haswa mwendo kasi ,yeyote atakae bainika ameuharibu hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Mohamed Mpinga  katika hafla ya kufunga kampeni ya abiria paza sauti iliyofanyika katika  katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo ambapo amesema kuwa mwendo kasi ni chanzo kikubwa cha ajali barabarani 

Kamanda amefafanua kuwa kampeni hiyo imeleta matokeo chanya ambayo imeonyesha kupungua kwa ajali ukilinganisha na miaka 25 iliyipita  nakusema kuwa Tanzania imepata mafanikio makubwa katika kuthibiti ajali za barabarani .

Amezitaja takwimu hizo kuanzia mwaka  2015 Desemba ajali zilikuwa 767 , Disemba 2016 ajali zilikuwa 705, ambapo januari 2016 ajali zilikuwa 681 hadi januari 2017 ajali zilikuwa 525, Februari 2016 ajali zilikuwa 846 ambapo februari 2017 ajali zilikuwa 455 ,kuna upungufu wa asilimia 46 'ambapo ajali zinazidi kupungua mwaka hadi mwaka. 

Ameendelea kusema kuwa kwa takwimu hizo hadi sasa Tanzania imepiga   kubwa katika kudhibiti ajali za barabarani na hii ni takribani nusu karne tangia mwaka 1989.
 
Kamanda Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na Madereva waliopendekezwa kama madereva bora 2016 - 2017 katika hafla ya kufunga kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyofanyika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, ambapo kampeni hiyo ilizinduliwa Novemba 2016 na Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Hamad Masauni ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani Tanzani.
 
Vile vile Kamanda mpinga alitoa vyeti vya pongezi kwa madereva walio pendekezwa kama madereva bora kwa mwaka 2016 - 2017 ambao ni;
1. AWADH BAWAZIR(RATCO).
2.ALLY ISSA (STAR BUS)
3. MUSTAPHA GHARIB(KIMBINYIKO)
4. DAUDI LWENA(KHANDAHAR). 
5. MENGI KASIKE(SUTCO).
6. MAJURA KAFUMU
 
Kwa upande wake mratibu na mwenyekiti wa abiria paza sauti  Asp.Mosi Ndozero  amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa madereva pamoja na wahudumu  wa magari sambamba na kuwaelimisha abiria kufahamu haki zao pia kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale wanapoona viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani ambavyo vinaweza kusababisha ajali na kupoteza maisha au ulemavu wa kudumu.

 Mosi amesema kuwa mtu anapopata ajali haathiriki yeye peke yake inajumuisha familia yake pamoja na serikali kuingia gharama kubwa ya  kumuuguza huyu mtu  aliyepata ajali,amewataka mabalozi kuendelea kupaza sauti kwa madereva bodaboda ambao wanapakiza mizigo kuzidi uwezo wa pikipiki pamoja na wale anaopakia Mishikaki.
 
Asp. Mosi Ndozero Mwenyekiti wa Kampeni ya Abiria Paza Sauti akizungumza katika hafla ya kufunga kampeni ya Abiria Paza Sauti iliyofanyika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, ambapo kampeni hiyo ilizinduliwa Novemba 2016 na Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Hamad Masauni ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani Tanzani.
Picha na Vero Ignatus & Murtadhwa Elbahsan