Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +25565373432 | +255778744123 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Wednesday, 19 April 2017

RSA - Zanzibar: Balozi Seif Ali Iddi Azindua Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Zanzibar............... Ashauri Sheria za Usalama Barabarani Ziongezwe Makali.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akionyesha cheti maalum baada ya kuweka saini yake cha kuthibitisha uzinduzi rasmi wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Zanzibar (RSA) hapo Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar. Wa kwanza kutoka kulia ni Naibu Kamishna wa Kikosi cha Usalama Bara barani Tanzania DCP Mohamed Mpinga, Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Waziri wa Ujenzi Balozi Ali Karume na Kamishna wa Polisi Zanzibar (CP) Hamdan Makame.


 Na Murtadhwa Elbahsan, Zanzibar.

 Matukio ya uvunjifu wa sheria za usalama Bara barani bado yanaendelea kupoteza nguvu kazi ya Taifa wakiwemo Vijana wazee na watoto huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu na wengi kuendelea kuwa mayatima katika maisha yao yote.

Akizindua rasmi Mtandao wa Mabalozi wa wa Usalama Bara barani Zanzibar hapo ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif Ali Iddi alisema hali hiyo imeendelea pia kuleta hasara kwa Taifa kutokana na kuharibiwa kwa miundombinu ya Bara bara na vifaa vyengine.

Balozi Seif alisema ajali za bara barani bado zimekuwa ni tishio kwa maisha ya wannchi kutokana na baadhi ya madereva ama kwa makusudi kutotii sheria na taratibu zilizowekwa katika kufuata matumizi sahihi yaliyowekwa bara barani.

Alisema baadhi ya madereva hao wamekuwa na tabia ya kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo wa kasi bila ya kujali watumiaji wengine mbali mbali kama watoto ambao nao wana haki ya matumizi ya bara bara hizo.

Balozi Seif alionyesha masikitiko yake kutokana na baadhi ya madereva ambao husababisha ajali za kizembe kutokana na ustaarabu wa kisasa ulioingiza wa kuendesha chombo cha moto na huku wanazunguza na simu wakati mataifa mengine Duniani hili wanalihesabu kuwa kosa kubwa bara barani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema uamuzi wa kuanzishwa kwa dhana hii ya mabalozi wa usalama Bara barani hapa Zanzibar ni wa busara na kuwa wakati muwafaka ambapo Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada za kukabiliana na ajali za bara barani.
 

  Mapema akitoa Tarifa Mwenyekiti wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani Nd. Mustafa Mussa alisema Mtando huo wa Kiraia umeanzishwa kwa lengo la kulisaidia Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama bara barani kupambana na na makosa yanayotokana na bara bara.

Naye Mlezi wa Mabalozi wa usalama Bara barani Msaidizi Kamishna wa Jeshi la Polisi (ACP ) Mkadam Khamis Mkadam alisema ajali nyingi zinazotokea Bara barani hutokana na vitendo visivyo tii sheria za usalama bara barani.

Alisema ajali za bara barani zilizotokeza mwaka 2016 zilifikia mia 604 na kusababisha vifo vya watu 147 wakati mwaka 2017 ziliripotiwa ajali mia 517 zilizosababisha vifo vya watu 133 kukiwa na upungufu wa vifa vya watu 14.

 


Balozi Seif akimkabidhi cheti Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Bibi Narsa Mohamed kutokana mchango mkubwa uliotolewa na vyombo vya habari vya Shirika hilo wa suala la usalama bara barani.
Balozi Seif akikabidhi cheti maalum kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Mabalozi wa Usalama Bara barani Tanzania Bwana John Seka kutokana na mchango mkubwa wa Taasisi hiyo uliosaidia kupunguza ajali za vyombo vya moto Bara barani Tanzania Bara.


Picha na – Elbahsan Blog ZNZ.

No comments:

Post a Comment