Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +25565373432 | +255778744123 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

Saturday, 8 July 2017

SIKU YA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI YAFANYIKA KITAIFA MKOANI DODOMA


Naibu waziri wa Ulinzi Mhandisi Hamad Masauni ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Taifa(Mwenye T-Shirt ya Blue) akiwa ameambatana na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini DCP Mohammed Mpinga ambae pia ni katibu wa Kamati ya usalama barabarani na Mlezi wa RSA Tanzania wakiwa wanaingia uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma baada ya kupokea maandamano ya Mabalozai wa usalama Barabarani yaliyofanyika mapema leo Mjini Dodoma (Makao makuu ya Nchi). Picha na Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus

 Na.Murtadhwa Elbahsan / Vero Ignatus 
Siku ya mabalozi wa usalama barabarani (RSA) imefanyika Kitaifa mkoani Dodoma ambapo Naibu waziri wa Ulinzi Mhandisi Hamad Masauni amekuwa mgeni  rasmi, shughuli hiyo imefanyika katika viwanja vya mashujaa na imewashirikisha mabalozi mbalimbali Tanzania bara na Visiwani.

Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama Taifa John Seka amesea kuwa lengo kuu la siku hiyo ni kuweza kuleta uhamasishaji kwa wananchi  ili waweze kupata elimu ya usalama barabarani na wasione ni jukumu la jeshi la polisi peke yake, kukuza mahusiano na jeshi la polisi  pamoja na mabalozi kufahamiana zaidi na kuwapongeza mabalozi kwa kazi nzuri ambayo wanayoifanya ya kujitolea. 

Kwa upande wake kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani  ambae pia ni katibu wa Baraza la usalama barabarani Taifa DCP  Mohammed Mpinga  amesema kuwa takwimuza vifo na majeruhi zinaonyesha kuwa nchi zinazoendelea zinaathirika sana na tatizo hili hivyo bado tunalo jukumu kubwa la  kupingana na ajali za barabarani
Ameainisha takwimu za ajali kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2017 zimepungua kwa asilimia 44  vifo vimepungua 13% majeruhi 30% ambapo wa asilimia kubwa RSA inahusika kwa kiwango kikubwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi  changamoto  kutambua juhudi za usalama barabarani wanaojitole.

Mpinga ambae  pia ni mlezi wa( RSA)amewapongeza mabalozi hao kwa kazi nzuri wanayoifanya  kwa kukabiliana na ajali za barabarani kwa kuonya kukaripia pale wanapoana mwenendo mbaya wa madereva pamoja na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani
“ Muendelee kujitoa kama vile ambavyo mnavyojitoa  kwani mnalirahisishia kazi jeshi ,mmekuwa mkiokoa maisha ya watu wasife kwa uzembe kwaajali za kujitakia “alisema .

Amezitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na vifaa vya lkutendea kazi,ubovu wa barabara na miundombinu,ukosefu wa alama za barabarani,utashi wa kisiasa ,wadau wanaona suala la usalama barabarani siyo la kwao na haliwahusu.

Mkuu wa kitengo cha Elimu nchini Tanzania ASP Mosi Boniface Ndozero  amesema kuwa mambo mawili lazima yazingatiwe, “ni vyema kuzingatia na kufuata alama za usalama barabarani yote yakizingatiwa ajali  zitapungua kabisa” amesema kuwa jeshi lapolisi nchini kitengo cha elimu limejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa elimu wanayoitoa  inawafikia walengwa pamoja na hayo amesema jeshi la polisi limejipanga  kutoa elimu kwa wanafunzi mashuleni kuhusu elimu ya usalama barabarani 

Kwa upande wake  Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP Lazaro Mambosasa  amesema kuwa wanamipango  endelevu  katika mji wa Dodoma  ili ujio wa serikali usije ukaongeza vifo na ajali kwani wamejipanga kuthibiti ajali za barabarani   

Ikumbukwe kuwa RSA imesajiliwa rasmi mwaka 2014 kama taasisi isiyo ya kiserikali ikiwa na wanacham 10 hadi sasa wapo zaidi ya 60,000 kwenye majukwaa ya mitandao wa kijamii (Whatsap, Facebook, Twitter, Instagram nk.), wapo wakurugenzi 8, kanda 5ambazo ni kanda ya kusini, kanda ya kati, kanda ya kaskazini ,kanda ya mashariki,kanda ya ziwa na kanda ya nyanda za juu kusini, wapo maadimini 20 kwenye majukwaa hayo ya mitandao ya kijamii.


Friday, 7 July 2017

KUELEKEA RSA DAY 8/7/2017 DODOMA. 
Na. Murtadhwa Elbahsan na Mustapha Mussa.
kilele cha maadhimisho ya RSA DAY (siku ya mabalozi wa salama Barabarani) tarehe 8/7/2017, leo hii mabalozi kutokea kanda ya mashariki ambayo inajumuisha mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro kwa pamoja wameanza safari ya kulelekea dodoma kwa ajili ya kufanikisha tukio hilo  muhimu kwa mabalozi wa usalama barabarani, pamoja na kuwa mabalozi wa kanda ya mashariki lakini wameambatana na balozi kutoka Zanzibar ambaye ata wawakilisha mabalozi kutokea visiwani humo. kwa ujumla  wao wanakamilisha idadi ya maalozi 44 kwenye msafara huo.

kupitia tamasha hilo la RSA DAY mabalozi wote nchi nzima watapata fursa ya kushirikishana uzoefu kuhusu masuala ya usalama barabarani, kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kuzuia ajali zinazo epukika na kuunga mkono juhudi za kuimarisha usalama barabarani, kujumuika pamoja na kujenga / kumarisha urafiki na mahusiano mema baina yao na kusajili mabalozi wapya wa usalama barabarani.

samba na yote kuanzia mwanzo wa safari hiyo watakuaa wakitoa elimu katika baadhi ya vituo vya mabasi kwa lengo la kutimiza wajibu wao kama mabalozi wa usalama barabarani.
Kauli mbiu "RSA ni familia moja, Hamasisha, Imarisha usalama barabaranni"

Picha na. Ramadhani Shabani

Mabalozi wakiwa ndani ya basi safarini kuelekea Dodoma (kushto ni Balozi Murtadhwa Elbahsan na Balozi Mustapha Mussa)

Balozi akiwa ndani ya basi safarini kuelekea Dodoma - Balozi Quen Moe

Mabalozi wakiwa ndani ya basi safarini kuelekea Dodoma

Mabalozi wakiwa ndani ya basi safarini kuelekea Dodoma
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana na mabalozi wa mkoa wa Morogoro walio ongozwa na Afande Sandey

Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana na mabalozi wa mkoa wa Morogorowalioongozwa na Afande Sandey


Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana na mabalozi wa mkoa wa Morogoro
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana na mabalozi wa mkoa wa Morogoro

Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana na mabalozi wa mkoa wa Morogoro
Saturday, 1 July 2017

RSA DAY 2017/SIKU YA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI
RSA TANZANIA inakuletea siku ya mabalozi wa usalama barabarani, tukio la aina yake ambalo linawapa fursa wadau wa usalama barabarani kukutana pamoja na kuonesha ari yao ya kuhamasisha wananchi kushiriki kuimarisha usalama barabarani, kwa kutoa elimu, kucheza michezo mbalimbali, na kutathimini hali ya usalama barabarani. Lengo ni kuhakikisha kuwa ajali nchini Tanzania zinakoma na wananchi wanatembea salama barabarani. 

Malengo ya RSA DAY 
 1. Kushirikishana uzoefu kuhusu masuala ya usalama barabarani
 2. Kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kuzuia ajali zinazoepukika na kuunga mkono juhudi za kuimarisha usalama barabarani
 3. Kutoa elimu ya usalama barabarani
 4. Kujumuika pamoja na kujenga urafiki na mahusiano mema
 5. Kusajili mabalozi wa usalama barabarani 

Taswira ya Tukio 
Jina la tukio: RSA DAY DODOMA 2017 
Aina: Tamasha 
Kauli mbiu: ”RSA ni Familia Moja. Hamasisha, Imarisha Usalama Barabarani”
Mhali: Uwanja wa Mashujaa 
Muda wa tukio: Siku nzima 
Tarehe ya Tukio: 8th July 2017 
Wahusika: Wadau wa Usalama Barabarani 
Waalikwa: Wananchi wote 

Shughuli za siku ya tukio
Shughuli zinazotarajiwa kufanyika siku hiyo zitahusisha; 
 1. Utoaji elimu stendi kuu ya Dodoma 
 2. Maandamano ya kuhamasisha ushiriki wa wananchi na wadau kwenye masuala ya usalama barabarani.
 3. Utoaji wa tuzo na vyeti.
 4. Mechi ya mpira wa miguu.
 5. Hotuba: • Mgeni rasmi, 
  • Mkuu wa Mkoa 
  • Mwakilishi wa RSA 
  • Mwakilishi wa wasafirishaji 
  • SUMATRA 
  • Jeshi la Polisi
 6. Kutoa elimu vituo vya bodabodas na bajaji 
 7. Kuvusha wananchi kwenye vivuko vya waenda kwa miguu 
 8. Nyimbo na michezo na
 9. Muziki 
Nyote mnakaribishwa katika siku hii adhimu ambayo licha ya kuwa ni siku ya furaha na burudani kwa mabalozi kukutana pamoja na kutathimini utendaji kazi wao kwa kipindi cha miaka mitatu, ni fursa nzuri ya kuelimisha wananchi kuhusu usalama barabarani na kuwafanya wachukue jukumu la kuhakikisha wanaenenda kwa usalama barabarani. 


KARIBUNI SANA.
RSA TANZANIA-USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.