Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +25565373432 | +255778744123 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

About Us

ROAD SAFETY AMBASSADORS - RSA

UTANGULIZI

RSA TANZANIA ni taasisi huru isiyo ya kiserikali inayojihusisha na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kuimarisha usalama barabarani. Kazi hi hufanywa kupitia elimu kwa umma, utoaji wa taarifa za uvunjifu wa sheria za Usalama Barabarani, pamoja na kushawishi mabadiliko ya tabia, sheria na sera. Taasisi ilianzishwa rasmi tarehe 28 Disemba 2014 na kusajiliwa rasmi tarehe 11 Novemba 2015, chini ya sheria ya makampuni sura ya 212, kama taasisi yenye udhamini, isiyo na mtaji na isiyogawana faida(a company limited by guarantee). Nambari ya usajili ya taasisi hii ni 121509.
 Hivyo basi, taasisi inatakeleza shughuli za kijamii bila malipo na katiba yake(Memorandum of Association) inahitaji kwamba mali pamoja na mapato yote ya taasisi vitumike pekee kwaajili ya kuwezesha malengo ya taasisi kama yalivyotanabaishwa katika katiba yake. Hakuna kiasi chochote cha mapato au mali kinachoweza kugawanywa kwa wanachama wake. Ili kujiendesha na kuwezesha kazi mbalimbali taasisi yetu inategemea Zaidi michango ya hiyari ya mabalozi na wanachama wake kwa ujumla. Ni lengo la RSA kujisajili kama asasi kamili ya kiraia chini ya sheria ya asasi zisizo za kiserikali(NGOs) kwa kupata cheti cha utimilifu(certificate of compliance).

UENDESHAJI WAKE

Kwakuwa taasisi imesajiliwa chini ya Ofisi ya Msajili wa Makampuni, sheria inataka taasisi hi iwe na wanachama, bodi ya wakurugenzi, menejimenti(yaani watendaji wa kila siku), mwanasheria, na kila mwaka ipeleke taarifa za mahesabu yake. Kwa ufupi RSA inapaswa kujiendesha kitaasisi Zaidi na kwa mujibu wa sheria, ambapo pamoja na mambo mengine taasisi itakuwa na mkutano mkuu, mikutano ya bodi na kukidhi mambo mengine ya kisheria.
Hivyo basi kwa mantiki hii ieleweke kwamba mtu yeyote anayetaka kuwa mwanachama wa RSA TANZANIA kwa mujibu wa sheria atapaswa kujaza fomu na kusajiliwa kuwa mwanachama kwa mujibu wa utaratibu utakaowekwa. Kuwa balozi tu peke yake haitatosha kuwa mwanachama. Na hii itasaidia sana uendeshaji wa taasisi, kutambuana, na kufanya kazi kwa ufanisi Zaidi. Aidha kwa sasa taasisi ina wadhamini wake wa kwanza kumi waliosaini waraka wa usajili kwa niaba ya mabalozi wote, na ndani ya hao wadhamini kumi, tisa kati yao wanaunda bodi ya wakurugenzi kwa mujibu wa sheria. Hivi sasa bodi ya wakurugenzi inaongozwa na Mwenyekiti wake John Seka. Katibu na Mwanasheria wa taasisi ni ndugu Wakili Adam Phillip, ambaye kwa sasa ndiye katibu wa Bodi.
Upande wa menejimenti ya RSA kuna muundo mpya wa uongozi kwa mujibu wa sheria (Organizations structure). Muundo huu sasa unatambua Mkutano Mkuu; Bodi ya Wakurugenzi; Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ya Bodi; Mwanasheria wa Kampuni (Company Secretary); Mkaguzi wa ndani Mahesabu; na Mtendaji Mkuu (Chief Executive Officer). Chini ya ofisi ya Mtendaji Mkuu kuna Mkurugenzi wa Fedha na Utawala ambaye chini yake kuna Afisa Tawala, Waratibu wa RSA Kanda (ZRCs) na Mhasibu; Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Tafiti na Utekelezaji wa Sheria ambapo chini yake kuna Afisa wa Tafiti na Afisa Utekelezaji; na Mkurugenzi wa Elimu, Habari na Mawasiliano ambapo chini yake kuna Meneja wa shughuli za mtandaoni, na mejena wa shughuli za nje ya mtandao. Chini ya ofisi ya meneja wa shughuli za mtandoni wanafuata admins wote, na chini ya ofisi ya Meneja wa shughuli za nje ya mtandao kuna kamati mbalimbali. Chini ya ZRCs kutaendelea kuwa na Kamati za Uratibu za Mikoa ambazo hivi sasa zinaongozwa na waratibu wa mikoa ambao tunawaita wenyeviti.

UWAZI NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU

RSA kama taasisi itaendelea na inatakiwa kuendeshwa kwa uwazi katika ngazi zote. Hii inahusisha upatikanaji wa nyaraka muhimu kama vile Mpango Mkakati (Strategic Plan); Kanuni na Muongozo Mkuu( RSA’s by law/Adminstrative Manual); Sera za Rasilmali watu; Manunuzi; Fedha; nk. Baadhi ya Nyaraka hizi zipo na nyingine zipo katika hatua ya kuandikwa na wataalamu mbalimbali na baadaye kupitishwa na bodi ya wakurugenzi. Baada ya tovuti yetu kukamilika na kuwa hewani zitapatikana kwenye tovuti. Lakini pia zitapatikana kwenye makavazi(Archive) yetu ya kule facebook, na blog tutakayoiunda baadae.
Kwa minajili ya mahesabu na ukaguzi, viongozi wote mnatakiwa kutunza kumbukumbu za miamala mbalimbali ikiwemo kuwa na risiti za kila muamala. Hatua hii imeenda sambamba na kupokea pes azote za RSA TANZANIA kupitia nambari 0716 000 515, na baadae kupitia akaunti ya benki. Kwa sasa RSA TANZANIA inayo akaunti katika benki ya Wanawake Tanzania(TWB) baadae itafunguliwa kwenye benki ambayo kila mwanarsa ataweza kubenki kiurahisi kutokana na mtandao wake wa matawi kuwa mkubwa. RSA TANZANIA kwa sasa inakamilisha kuwa na vitabu vya risiti, fedha, nk ili kuendana na kanuni zake za fedha. Baada ya nyaraka hizo kukamilika kila fedha itakayopokelewa itakatiwa risiti, fedha itatolewa kwa kuombwa, makusanyo na matumizi yote yatakuwa yakikaguliwa. Hivyo wanarsa wote tunatakiwa tuanze kuzoea mfumo huu mpya wa kiutendaji. Viongozi watakuwa wakipewa maelekezo ya mara kwa mara. Tutaendelea kukutana katika mikutano, tutapokea maoni, uboreshaji nk ili kuifanya taasisi yetu isonge mbele. Kuanzia mwenzi Januari 2017 fomu za usajili wa wananchama rasmi  wa rsa zitaanza kutumika na kila mmoja atapata fursa ya kuzijaza na hatimaye kupewa kitambulisho.

OFISI

Kwa sasa ofisi sajiliwa ya RSA TANZANIA ni kupitia ofisi ya mwanasheria wake bwana Adam Phillip iliyopo Jengo la Jued Masaki, lakini ofisi inayoratibu mipango na mikakati mbalimbali ipo katika stendi ya Makumbusho, Kinondoni jijini Dar es Salaam, karibu na mnara wa intaneti (wifi) stendi hapo. Mnakaribishwa sana kupita ofisini kupafahamu. Hata hivyo, mipango ya baadae ni kuhamisha ofisi mahali hapo kutokana na kuwa na ufinyu wa sehmu za kuegesha magari na vitu vingine. Ofisi yetu inahudumiwa na afisa tawala Queen Paul Moe, Mhasibu ndugu Frederick Wambura na Afisa Takwimu Bi, Irene Msellemu. Watu hawa wanafanya kazi kubwa sana ya kujitole kuhakikisha RSA inasimama imara kama taasisi.
Kutokana na uchanga wetu kama taasisi(mwaka mmoja tu tangu usajili) bado hatuwezi kufanya mambo makubwa sana, mf.kuwa na ofisi kubwa nzuri kwani hatuna pesa ya kulipia pango la hadhi hiyo, samani nk. Hivyo, mabalozi bado mnapewa mwito kuchangia ukuaji wa taasisi hii kwa kutoa samani, fedha, au aina yoyote ya ufadhili kuwezesha shughuli za taasisi kusonga mbele. Mbele ya safari tutahitaji boda boda au bajaji kwaajili ya kuwezesha kusukuma shughuli zetu mbele. Mwaka huu kazi kubwa sana imefanyika kuweza kutengeneza nyaraka mbalimbali ili RSA isimame kitaasisi Zaidi.

UFADHILI

Hadi sasa RSA TANZANIA haina mfadhili rasmi yeyote yule Zaidi ya kutegemea mabalozi wake wenyewe ambao hata hivyo michango yao ya kifedha haikidhi sana. Tunawashukuru sana kwa moyo huo. Hata hivyo tayari wafadhili mbalimbali wameshaonesha nia ya kutaka kufadhili shughuli za RSA, kama vile Foundation for Civil Societies, Global Road Safety Partnership, Buzwagi Gold Mine, CRDB nk. Hawa ni baadhi tu ya taasisi ukiacha taasisi kama SUMATRA na Baraza la Taifa la Usalama Barabarni ambao tumekuwa nao mara kwa mara. Ili taasisi hizo ziweze kufadhili shughuli zetu ni lazima tukidhi masharti na vigezo vingi ikiwemo kuwepo na uongozi thabiti, kuweka kumbukumbu za mahesabu vizuri, kuwa na utaratibu mzuri wa malipo na matumizi ya fedha; kuwa na nyaraka mbalimbali kama vile mpango mkakati, sera ya fedha na manunuzi, sera ya rasilmali watu, andiko la mradi mnaotaka kuombea fedha nk. Kazi zote hizi kuzifanya zinahitaji rasilmali watu na fedha. Tunawashukuru sana watu wote wanaojitole rasilmali fedha na akili zao wenyewe kutusaidia kuandika baadhi ya nyaraka. Shukrani sana kwa bwana Arif Lardhi mlezi wa RSA Kanda ya Mashariki kwa kusaidia kutengeneza vitabu vya risiti na fedha kwaajili ya RSA kanda hiyo; Silas Bwire kwa kutengeneza Mpango mkakati wa vyombo vya habari (RSA Media strategy), John Seka kwa kuandika andiko la mradi wa Child Restraint na Seatvelt; wakurugenzi wote kwa kuwa na michango ya kila mwezi, kwaajili ya uendeshaji wa ofisi, nanyi mabalozi wote kwa michango yetu mbalimbali bila kuchoka.

UTENDAJI KITAALAMU ZAIDI

RSA TANZANIA lazima tuendeshe shughuli zetu kitaalamu Zaidi. Lazima tujitofautishe na taasisi nyingine, katu hatupaswi kuwa wababaishaji. Badala ya kuwa wapiga kelele sisi tuwe watu wa KUJENGA HOJA ZENYE MASHIKO NA USHAHIDI, Kama ni malalamiko basi yawe yenye tija ambayo mtu hahitaji kurumia darubini kuona kuwa malalamiko haya ni ya kweli. Aidha, tuwe watu wa kufanya tafiti za kitaalamu na zenye ushawishi miubwa wa kuishauri serikali namna bora ya kukabiliana na ajali za barabarani. Tushiriki kwa dhati katika kukabiliana na ajali za barabarni. Lugha zetu ziendelee kuwa zenye staha lakini zinazofikisha ujumbe stahiki kwa wahusika. Tusihangaike Zaidi na kujisifu kwa kazi zetu bali tuuachie umma utuhukumu kwa kazi zetu na kutusifu kwa yale mazuri tufanyayo. Kama taasisi hatupo kwenye mashindano na taasisi yoyote bali tupo kwenye mashindano na ajali za barabarani, lengo letu kusiwe na ajali kabisaa. Tujitolee kwa dhati kwani RSA ni ibada. Kila mmoja katika RSA ana mchango wake na tunauthamini sana. Kila chombo kitafanya maamuzi kulingana na mamlaka yake, nasi kama mabalozi tuheshimu maamuzi ya vyombo vyetu mbalimbali, tukosoe pale inapobidi, lakini kosoa yetu iwe ya kujenga na sio kulenga kubomoa au kuidunisha RSA TANZANIA.

VISION(DIRA) NA MISSION (DHIMA)  AMBAZO NI:

Dhima (Mission)
Kuimarisha usalama barabarani kupitia utoaji wa elimu na taarifa za usalama barabarani, kuhamasisha ushiriki hai wa umma; pamoja na mabadiliko ya sheria na sera.
Dira (Vision)
Kuwa na jamii ambayo Usalama Barabarani ni Suala la Kipaumbele

BODI YA WAKURUGENZI

1. John Seka
2. Asina Omary
3. Augustus Fungo
4. Johansen Kahatano
5. Mohammed Mpinga
6. Ally Nurdin
7. Gibson Urassa
8. Adam Phillip
9. Jackson Kalikumtima

VIONGOZI MBALIMBALI KWENYE KURUGENZI YA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO YA RSA TANZANIA

ORODHA YA ADMINS WA TAIFA [NATIONAL ADMINS ROLL]

Admin1&Director IEC: Augustus Fungo
Admin2&Manager Digital Platforms: Jackson Kalikumtima
Admin3&Acting DIEC: Ally Nurdin (Six)
Admin4: Rama Msangi
Admin5: David Shao
Admin6: Khalid Shekoloa
Admin7: Stella Rutaguza
Admin8: Abel Ntaho
Admin 9&DA1: Siraj Sauko
Admin10&DA2: Gasper Kisenga
Admin11: Hussain Khalfan
Admin12: John Kelvin
Admin13: Vedastus Bulemo
Admin14: Leila Bhanji
Admins hawa watawajibika kwa uongozaji wa kila siku na mara kwa mara Kwa groups za RSA TAIFA.

Administrators: Twitter, Instangram and Facebook Official Page

1. Damasy Antony-Incharge RSA Facebook Official Page
2. Michael Vitalis- Incharge Instagram page
3. Chief  Murtadhwa Elbahsan-Incharge Twitter page
4. Jensen Nyerere-Moderator RSA Telegram

Administrators RSA SOCIAL Group on Telegram

1. Leila Bhanji
2. Alex Kakondele
3.Abuu Haji Kwaji

Waratibu Mbalimbali

Paza Sauti Project Coordinator: Queen Paul Moe
Data Management Officer &Admin without Portfolio: Irene Msellem-DMO/AWP
Coordinator Designs & Publications: Rama Msangi
Web Masters: Rama Msangi & Chief  Murtadhwa Elbahsan
Media Strategist1: Silas Bwire
Media Strategist2: Saumu Mwalimu
Media Strategist 3: Michal Vitalis

Note: ZRCs, Viongozi wa Kitaifa na Mikoa wote wanabaki kama walivyo na automatically wanakuwa admins kwa nafasi zao. Uteuzi mwingine utaendelea kadiri inavyofaa.

BAADHI YA KANUNI ZA RSA TANZANIA

Katika majadiliano yoyote yanayoendeshwa katika majukwaa ya RSA, yawe ya mtandaoni au ya nje ya mtandao, kila RSA atazingatia kanuni na miongozo ifuatayo:


1. HABARI SAHIHI:

Hairuhusiwi kuandika habari yoyote isiyo ya ukweli ama ya kufikirika tu na kuipa uhai kuwa ya kweli.
2. UHAKIKA WA TAARIFA:
Thibitisha taarifa kabla hujaituma na kama huna uhakika sema “sent as received, for verification”au “Habari hii Haijathibitishwa”. Hapa utaeleweka kuwa unataka jambo lifuatiliwe kujua ukweli wake na kwamba wewe si chanzo halisi cha taarifa.
3. UKAMILIFU WA TAARIFA:
Ripoti tukio kwa kutoa taarifa inayojitosheleza kwa kutaja nani muhusika (jina/namba ya gari/uelekeo), nini kimetokea, wapi limetokea, na ungependa nini kifanyike.
4. HABARI ZILIZOKATAZWA:
Ni marufuku kupost habari zinazohusu siasa, vichekesho, matangazo ya kibiashara, michezo, muziki, dini au habari binafsi labda kama zimetokea barabarani mf.ajali, homa, kuibiwa, breakdown, na kubambikiwa kosa/jinai. Kama huna hakika na habari tafadhali, mtumie admin inbox kwanza.

5. PICHA:
Hairuhusiwi kuweka picha mbaya za ajali zisizowastahi marehemu. Picha yoyote unayoweka humu au video sharti iwe ina maelezo yanayojitosheleza kuelimisha au kuchukua hatua. Pia si ruksa kurudia rudia mara nyingi kutuma picha hizo hizo au zinazotoa ujumbe mmoja iwapo ulizotoa awali zinajitosheleza.
6. KAULI/LUGHA YA MAWASILIANO:
Lugha ya Matusi, vijembe, siasa hairuhusiwi katika foram za RSA, wala ubishi usio wa hoja. Siku zote usinungĂșnike, lalamika kwa kutoa hoja na ikiwezekana pendekeza suluhisho.

7. SIRI/USALITI:
Kila rsa ana wajibu wa kutunza siri za kundi zinazohusiana na taarifa za uvunjifu wa sheria za barabarani.

8. VITISHO:
ni marufuku rsa yeyote kujaribu ama kumtisha mwenzake inbox au kwa sms au kwa simu au njia nyingine yeyote ila kwa sababu tu ya jambo alilolisema au taarifa aliyoitoa humu inayoenda kinyume na maslahi ya mtishaji au mtuhumiwa.

9. MARUFUKU:
Ni marufuku kwa RSA yeyoye kutumia Uanachama wake kwaajili ya kulinda maslahi yake binafsi, kutisha, kudhoofisha juhudi za RSA, kupotosha, kutotii sheria, kuomba upendeleo maalumu, kudhalilisha au kuhujumu juhudi zozote za RSA.Kufanya hivyo ni kosa na hatua za kinidhamu zitachukuliwa mara moja.

10. MAHUSIANO MEMA:
WanaRSA wote ni watu wanaoheshimiana na kupendana, na popote wanapokutana wanasalimiana na kubadilishana mawazo.

11. ADHABU:
Ukikiuka kanuni hizi utaadhibiwa kwa kutolewa kwenye kundi na unaweza kushtakiwa kijinai.


NB:
Admins wanayo haki ya kufuta post au maoni yoyote yanayokinzana na lengo la kundi. Katika kundi hili unashauriwa kutumia lugha ya staha katika kutoa malalamiko au kujenga hoja au kuuliza swali. Hapa tunabishana kwa hoja zenye ushahidi na sio siasa. Karibuni sana

This Blog Powerd by:
  Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of  Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 778 246 889
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment