Powered by: Elbahsan Web & Blog Designer
Do want your Network!!! Website or Blog-Spot, Try Us: Elbahsan Web & Blog Designer Contact Us Now... Calll; +25565373432 | +255778744123 Email; murtadhaalbahsan@gmail.com

ProjectsUtangulizi.

ABIRIA PAZA SAUTI ni kampeni ya usalama barabarani yenye lengo la kumjengea uwezo na kumhamasisha dereva na abiria kuchukua tahadhari kuepuka ajali bila uwepo wa polisi. Kampeni inalenga kumfanya abiria atambue haki na wajibu wake akiwa kwenye basi; apaze sauti pale kunatpotokea uendeshaji hatarishi barabarani, na tatu kumfanya dereva abadili mtazamo wake na kujenga utamaduni wa usalama barabarani. Hii inamfanya dereva kuwa sehemu ya suluhisho la ajali za barabarani.
Mradi wa ABIRIA PAZA SAUTI unatekeleza mikakati miwili kati ya mitano ya kuzuia ajali Tanzania kama ilivyo ainishwa katika sera ya taifa ya usalama barabarani, 2009. Mikakati hiyo ni Uhandisi na mazingira ya barabara; Elimu na taarifa; Usimamizi na sheria; Mwitikio wa dharula; na Tathmini na masuala mtambuka. Kampeni ya ABIRIA PAZA SAUTI imejikita katika eneo la Elimu na taarifa na eneo la Usimamizi na sheria. Sera inaainisha kuwa bado kuna uelewa mdogo wa umma kuhusu usalama barabarani hivyo kuna haja ya polisi na wadau wengine kushirikiana kuhakikisha kuwa elimu inaufikia umma. Aidha mapungufu ya sheria na usimamizi hafifu unatajwa kuwa kati ya changamoto zilizopo katika kuimarisha usalama barabarani. Kampeni ya Abiria Paza Sauti pia inakuja kuimarisha usimamizi wa sheria na kuainisha mapungufu yaliyopo ili yafanyiwe kazi.
Kampeni hii ni muendelezo wa kampeni kama hii iliyofanyika mwezi Novemba na Disemba mwaka 2015 kwa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na RSA TANZANIA. Kampeni hii itaendeshwa kwa awamu mbili za miezi mitatu mitatu, awamu ya kwanza ikiwa mwezi Novemba hadi January na awamu ya pili ikiwa mwezi februari hadi Aprili. Kampeni itaendeshwa na mabalozi wa RSA na wale wa taasisi nyingine walioenea kote nchini.

LENGO KUU LA KAMPENI

Lengo kuu la kampeni ni kuhamasisha ushiriki timamu wa wananchi katika kuzuia ajali za barabarani kwa kuchukua hatua stahili wakati sahihi bila ya uwepo wa askari polisi.

Malengo mahsusi
Malengo mahsusi ya kampeni ni:
(a) Kumfanya dereva atii sheria bila shuruti
(b) Kubadili mtazamo wa abiria na madereva kuhusu usalama barabarani
(c) Kumjengea uwezo abiria kuzungumza bila woga kukemea udereva hatarishi barabarani
(d) Kumwelimisha abiria kuhusu haki na wajibu wake barabarani na baada ya ajali.


MATOKEO TARAJIWA

(a) Kuimarika kwa hali ya usalama barabarani
(b) Madereva kubadili tabia zao na kuwa wazingatiaji bila shuruti wa sheria
(c) Wananchi kuwa na uelewa mpana kuhusu usalama barabarani.


VIASHIRIA VYA MAFANIKIO

(a) Kupungua kwa idadi ya ajali zinazotokana na makossa ya kibinadamu
(b) Idadi ya abiria wanaofunga mikanda kuongezeka
(c) Ushuhuda wa madereva na makondakta kuwaelekeza na kuwahimiza abiria kufunga mikanda
(d) Kuongezeka kwa idadi ya ripoti kutoka kwa wananchi kuhusu uvunjaji wa sheria na kudai haki zao mbalimbali
(e) Kupungua kwa idadi ya makossa ya upitaji mbaya wa magari na mwendokasi kwa madereva walioteuliwa

SHUGHULI KUU ZA KAMPENI

(a) Kutengeneza muungano (coalition) wa wadau watakaohusika na kampeni ya ABIRIA PAZA SAUTI
(b) Kuongea na waandishi wa habari (Press conference) kuwaeleza kuhusu kampeni
(c) Kufanya Uzinduzi wa kampeni kitaifa Ubungo Bus Terminal Dar es salaam
(d) Kupanda kwenye mabasi na kutoa elimu
(e) Kuwafuata waendesha pikipiki na kuwaelimisha
(f) Kuwafuata wanavijiji waishio kandoni mwa barabara kuu  na kuwaelimisha
(g) Kuwa na warsha na madereva 100 watakaoshiriki katika kampeni
(h) Kuwafuatilia madereva kwa kuchukua taarifa zao kutoka polisi na SUMATRA
(i) Kuweka kumbukumbu za picha na vielelezo mbalimbali kila shughuli ya kampeni inapofanyika
(j) Kuwazawadia madereva bora mwishoni mwa kampeni

WASHIRIKI

Kampeni itashirikisha wadau wote muhimu yaani RSA, CHAKUA, POLISI, ZIMAMOTO, SUMATRA, KAMATI ZA USALAMA BARABARANI MIKOA,SUMATRA CCC, UWAMATA, TABOA, na MAKINI APP.

WANUFAIKA WAKUBWA

Wanufaika wakubwa wa mradi huu ni madereva na abiria, japokuwa mradi utawafikia watu wengi Zaidi ya abiria na dereva.

MBINU

Kampeni itatumia mbinu zote muhimu kufanikisha lengo lake, baadhi ya mbinu hizo ni kuendesha vipindi vya uelimishaji kwenye vyombo vya habari, kufanya ukaguzi wa vyombo vya usafiri kubaini mapungufu na kutaka marekebisho yafanyike, askari kuchukua hatua dhidi ya wavunjifu wa sheria; kupanda mabasi na kuelimisha; kutembea katika shule, vyuo, na vituo vya pikipiki na kuelimisha.This Blog Powerd by:
  Elbahsan Web & Blog Designer
A Subsidiary of  Elbahsan Web & Blog Designer for Global Development, Inc.
+255 (0) 653 373 432 & +255 (0) 778 246 889
For the Web & Blog Template and Designing
Dar Es Salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment